Swahili The Muslims' COVID-19 Handbook 2

SWAHILI
KIJITABU CHA WAISLAM KUHUSU
COVID-19

MWONGOZO WA JINSI YA KUKABILIANA NA GONJWA LA COVID-19

KWA MTAZAMO WA KIISLAMUKIMECHAPISHWA KWA MASHAURIANO YA  WANAZUONI WA NGAZI ZA JUU NA MADAKTARI WA TIBA

Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu. Tunaomba msaada kwake, baraka na uongofu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu Mtume Muhammad, amlinde na amuinue katika daraja la juu.


Mlipuko wa janga la corona umeenea haraka ulimwenguni kote, na kubadili kabisa hali za maisha ya watu. Hii pia inajumuisha jamii ya kiislamu, ambayo imeathirika kwa njia tofauti.


Kwa kuandika kijitabu hiki, tunadhamiria kuleta matumaini kwa jamii kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kutoa vidokezo vya vitendo ambavyo vimewekwa katika kanuni na maarifa sahihi ya Uislam.


Malengo ya kijitabu hiki ni:

  • Kuimarisha imani zetu na mauhusiano yetu ya kiroho na Mwenyezi Mungu katika wakati huu.

  • Kuhakikisha tuko tayari kukabiliana na matukio yote juu yetu na wapendwa wetu.


Mwenyezi Mungu aufanye wakati huu wakati ambao tunakuwa karibu zaidi naye. Tunaomba atulinde, wapendwa wetu na jamii kwa ujumla kutokana na madhara. Mwishowe, tunamwomba awasamehe wale wote ambao wametangulia na awe na huruma juu yao.